Peaty atwaa medali ya pili ya dhahabu

Image caption Bingwa wa mchezo wa kuogelea Adam Peaty

Muingereza Adam Peaty ametwaa medali ya pili ya dhahabu katika michezo ya kuogelea ya dunia.

Peaty ameshinda katika mbio za mita 50 na kuwa mwanamichezo wa kwanza kushinda michezo miwili tofauti ya mita 50 na mita 100.

Nyota huyu wa mchezo wa kuogelea mwenye miaka 20 pia ameisaidia timu ya mchanganyiko ya Uingereza kushinda medali ya dhahabu na kuweka rekodi ya dunia katika mchezo wa kuogelea huko Kazan.

Uingereza imekua nchi ya tatu katika michuano hii kuweka rekodi ya dunia katika timu ya mchanganyiko ikiwa haihusishi michuano ya Olimpiki.

Jumla ya rekodi kumi za dunia zimewekwa katika michuano hii ya dunia ya mchezo wa kuogelea.