Mourinho:Madaktari wetu ni ''wajinga''

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mourinho:Madaktari wetu ni ''wajinga''

Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amewashambulia madaktari wa timu yake kuwa ni 'wajinga'' baada yao kutumia muda mrefu kumtibu Eden Hazard uwanjani mabingwa hao watetezi wa ligi kuu ya Premia ya Uingereza walipokuwa wakikabiliana na Swansea jana usiku huku wakiwa na mchezaji mmoja zaidi yao.

The Blues, ambao tayari walikuwa keshampoteza kipa Thibaut Courtois aliyekuwa kaoneshwa kadi nyekundu kwa kumwangusha mshambuliaji Bafetimbi Gomis walisalia 9 uwanjani baada ya timu ya utabibu kukimbia kushughulikia mguu wa Hazard na wakachukua muda mrefu japo kulingana na Mourinho hakukuwa 'ameumia sana''

''kwa kweli sikufurahia kauli yao ya kumtibu Hazard,ilitulemaza na kuwapa Swansea fursa ya kutushambuliwa maanake walikuwa na watu wawili zaidi yetu'' alifoka the Special one''

Haki miliki ya picha PA
Image caption Thibaut Courtois alioneshwa kadi nyekundu kwa kumwangusha mshambuliaji Bafetimbi Gomis

''Hapa uwanjani uwe ni mbeba mpira, daktari ama hata katibu mwandishi sharti uwe unafahamu jinsi mpira unaendelea uwanjani''

''Kabla ya kuingia uwanjani sharti ufahamu hali halisia kuwa tumekosa mchezaji mmoja na kuingia kutasababisha mwengine aondoke uwanjani''

''Nina hakika Eden hakukuwa katika hali mahututi ilikuwa tu ni kugongwa kidogo ,angeweza kuvumilia,kila mtu alikuwa amechoka '' aliongezea Mourinho

Mourinho alikuwa akizungumzia kisa uwanjani Chelsea walipokuwa nyuma dhidi ya Swansea huku wakiwa na wachezaji 10 kisha Hazard, akaangushwa na Gylfi Sigurdsson.

Wakati huo zilikuwa zimesalia dakika 6 pekee mechi hiyo kukamilika ndipo watabibu wa timu wakaingia kumsaidia walipomuona akichechemaa.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amewashambulia madaktari wa timu yake kuwa ni 'wajinga'' kwa kumtibu Eden Hazard uwanjani Swansea ilipokuwa na mchezaji mmoja zaidi

Chelsea ndio walikuwa wa kwanza kucheka na wavu kupitia mkwaju wa free-kick uliopigwa na Oscar kunako dakika ya 22 kisha

Andre Ayew akaisawazishia Swansea dakika saba baadaye.

Federico Fernandez alijifunga mwenyewe baada ya kutapatapa na mkwaju uliopigwa na Willian na kufanya mambo kuwa 2-1.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Bafetimbi aliihakikishia Swansea alama moja ya kufungua msimu alipofunga na kufanya mambo kuwa Chelsea 2 Swansea 2.

Lakini mambo hayakuishia hapo, Swansea walikuwa na ari ya kuzoa alama zote tatu na juhudi zao zilizaa matunda baada ya kipa wa Chelsea

Courtois kumuangusha Bafetimbi mbele ya lango na refarii akapuliza kipenga akiashiria ni penalti.

Kipa wa mpya wa ziada wa Chelsea Asmir Begovic alijipata uwanjani bila kupenda baada ya Courtois kuoneshwa kadi nyekundu kunako dakika ya 55 ya kipindi cha pili.

Bafetimbi aliihakikishia Swansea alama moja ya kufungua msimu alipofunga na kufanya mambo kuwa Chelsea 2 Swansea 2.