Wenger:Ushindi wa West Ham ni 'ajali'

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wenger

Klabu ya Arsenal nchini Uingereza imesema kuwa itajikaza na kukabiliana na 'ajali' waliopata baada ya kushindwa kwa mabao 2-0 na klabu ya West Ham siku ya jumapili.

Mkufunzi wa kilabu hiyo Arsene Wenger amesema kuwa timu yake ilipata jereha baya ambalo ni lazima ijipone.

''Tutakabiliana na kidonda tulichopata'', alisema Wenger.

Licha ya kumiliki mpira kwa asilimia 62 na kupiga mikwaju 22 katika lango la upinzania Arsenal ilishidwa 2-0 na wageni wao West Ham katika uwanja wa Emirates.

Wenger:Nilijua huenda ikawa mechi ngumu,lakini iwapo unajua huwezi kushinda mechi basi hakikisha kuwa hupotezi.