Pedro Rodriguez awabeba Barcelona

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Pedro Rodriguez akiwa kazini

Mchezaji aliyeingia kutokea benchi Pedro Rodriguez aliifingua timu yake bao la ushindi katika dakika za nyongeza ambapo Barcelona walishinda kombe la Eefa Super Cup mchezo uliopigwa kwenye mji wa Tbilisi.

Washindi wa kombe la Europa Sevilla waliwashangaza Bacelona ambao ni washindi wa klabu bingwa barani ulaya baada ya Ever Banega kufunga goli la kwanza kwa mkwaju safi wa adhabu ndogo.

Lionel Messi alifunga mara mbili na kuifanya Barca kuongoza kwa goli 2-1 kabla ya Rafinha na Luis Suarez kufumania nyavu na hivyo matokeo kuwa 4-1. Mabao ya Jose Antonio Reyes,Kevin Gameiro na Yevhen Konoplyanka yaliufanya mchezo huo kwenda dakika 30 za nyongeza kabla ya Pedro kuifungia Barca goli la ushindi.

Haya ni mafanikio makubwa kwa Barcelona tokea mwaka 2011 baada ya kushinda mataji matano mfululizo na kuwa sawa na klabu ya AC Milan ya Italia yenye rekodi sawa na hiyo.