Jack Wilshere mapema zaidi

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Jack Wilshere

Meneja wa Arsenal Mfaransa Arsene Wenger amesema kuwa kiungo wa klabu yake Jack Wilshere anatarajiwa kurejea tena dimbani wiki mbili zijazo baada ya kupata maumivu ya kifundo cha mguu.

Wilshere mwenye miaka 23 aliumia katika mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya Agosti 1 ambapo ilidhaniwa angekaa nje ya uwanja kwa miezi miwili. Lakini Wenger amesema kiungo huyo wa kimataifa wa Uingereza anatarajiwa kupona ndani ya muda mfupi ujao.

Wakati huo huo mchezaji mwenzake Tomas Rosicky aliyefanyiwa upasuaji wa goti anatarajiwa kukaa nje ya dimba kwa miezi miwili. Akiongea kabla ya kukutana na Crystal Palace katika mchezo wa jumapili, Wenger alisema ''Jack atakua nje kwa wiki nne na tiyari zimepita wiki mbili anaendelea vizuri''

Kiungo Rosicky mwenye miaka 34 aliumia mwezi juni alipokua akiitumikia timu yake ya Jamhuri ya Czech iliyomenyana na Iceland katika michuano ya kufuzu Euro 2016.