Tottenham yamsajili N'jie wa Cameroon

Image caption Clinton Njie

Klabu ya Tottenham imemsajili mshambuliaji wa Cameroon Clinton N'jie kutoka kilabu ya Ufaransa ya Lyon.

Mchezaji huyo wa miaka 22 ambaye ameandikisha kandarasi ya miaka mitano katika uwanja wa White Hart Lane hadi mwaka 2020,alisema;Niko tayari kuonyesha umahiri wangu ili kuisaidia kilabu hii kuafikia malengo yake.

N'jie aliifungia mabao 7 timu hiyo ya Ligi ya dara la kwanza msimu uliopita na pia ameifungia Cameroon mabao sita katika mechi 10 alizocheza.

Kuwasili kwake kunafuatia kuondoka kwa mshambuliaji wa Uhispania Roberto Soldado aliyehamia Villareal.