Chelsea yamsajili Baba Rahman

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Beki wa Klabu ya FC Augsburg, Abdul Rahman Baba

Klabu ya soka ya Chelsea imemsajili beki Abdul Rahman Baba kutoka klabu ya FC Augsburg ya Ujerumani.

Chelsea imethibitisha kukamilisha usajili wa beki huyo raia wa Ghana mwenye umri wa miaka 21 katika tovuti ya timu hiyo.

Usajili huu umefanyika kuziba nafasi ya beki wa kushoto baada ya Mbrazil luis Filipe kurudi katika timu yake ya zamani ya Atletico Madrid

Kocha wa Chelsea Jose Mourinho,anaamini mlinzi huyo ataleta ushindani kwa Cesar Azpilicueta katika nafasi ya beki wa kushoto.

Rahman ametumia muda wa miezi 12 na klabu ya Augsburg ambako alisajiliwa akitokea timu ya SpVgg Greuther F├╝rth Agosti mwaka 2014.