Asli Cakir Alptekin kuvuliwa medali

Image caption Asli Cakir Alptekin

Mshindi wa medali ya dhabau ya michezo ya Olimpiki mwaka 2012,Asli Cakir Alptekin amevuliwa ushindi wake baada ya kuhusika na matumizi ya dawa za kusisimua misuli.

Mkimbiaji huyo wa Uturuki pia amefungiwa kwa miaka nane kujihusisha na michezo hiyo, mahakama ya usuluhishi michezoni imedhibitisha.

Rufaa ya juu ya kesi hiyo inayomkabili mwanadada huyo mwenye miaka 29 ilisafishwa mapema nchini Uturuki.

Baada ya mbio hizo, Muingereza Lisa Dobriskey, aliyemaliza nafasi ya tisa katika mbio hizo aliiambia BBC ''Sikuamini kama nlikua nakimbia uwanjani pekee'' Alptekin alishinda hukumu ya kufungiwa miaka miwili baada ya vipimo vya awali kuonyesha hakuwa anatumia dawa hizo mwanzoni mwa mwaka 2014.

Matokeo yake ya ushindi tokea Julai 2010 yametenguliwa baada ya vipimo kuthibitisha kuwa alijihusisha na matumizi ya dawa hizo zilizopigwa marufuku michezoni.