Michuano mpira wa kikapu kuanza Tunisia

Image caption Mataifa 16 barani Afrika kushiriki Afrobasket

Michuano ya mpira wa kikapu kwa mataifa ya Afrika maarufu kama Afro basket yataanza kutimua vumbi leo nchini Tunisia.

Michuano hii itaanza Agosti 19 mpaka Agosti 30 huku mataifa 16 ya barani Afrika yakishiriki michuano hii mikubwa ya mchezo wa mpira wa kikapu.

Angola ndio mabingwa watetezi wa michuano hii ubingwa walioutwaa mwaka 2013 michuano hiyo ilipofanyika nchini Ivory Coast.

Mashindano haya kwa mara ya kwanza yalifanyika nchini Misri mwaka 1962. Nchi zinazoshiriki michunao hii ni wenyeji Tunisia Nigeria, Uganda, CAF ,Senegal, Angola na Mozambique.

Pia kuna Morocco,Egypt,Mali,Cameroon,Gabon, CIV,Zimbabwe,Cape Verde na Algeria.