Kevin de Bruyne amkera wakala wake

Wakala wa mshambuliaji wa Wolfsburg Kevin de Bruyne aitwaye Patrick de Koster amekasirishwa baada ya mchezaji huyo kuzungumzia mipango yake ya baadaye wakati wa sherehe za tuzo.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji aliombwa kurudia maneno ya mshereheshaji aliposema''Ni dhahiri kuwa nitachezea Wolfsburg msimu huu''. Patrick de Koster baadae alizungumza kwa jazba na BBC na kusema kuwa hakuna maamuzi yaliyofanywa juu ya hatima ya mchezaji huyo mwenye miaka 24. Manchester City wanatarajia kumsajili mchezaji huyo kwa dau la Euro milioni 40.