Ligi kuu Tanzania kuanza Septemba

Image caption Ligi kuu bara kuanza tarehe 12 mwezi Septemba

Ligi kuu ya Tanzania itaanza kutimua vumbi hapo Septemba 12, katika viwanja tofauti na kufikia tamati Mei saba mwaka 2016.

Jumla ya timu 16 ,zitashiriki ligi hiyo ambayo itachezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini.

Shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania (TFF), limevitaka vilabu vyote kukamilisha usajili wa wachezaji na viongozi kabla ya kufungwa kwa dirisha leo hii.

klabu ambayo haitawasilisha malipo ya ada ya mchezaji wa kigeni ya dola elfu mbili mchezaji huyo hataruhusiwa kucheza kwenye ligi hadi malipo hayo yatakapofanyika.

Michezo saba itachezwa siku ya ufunguzi jumamosi katika viwanja tofauti.