Valencia, Celtic na Shaktar zapeta

Image caption Valencia,Celtic,Shaktar zapeta

Valencia, Celtic na Shaktar zimeshinda kwenye Michezo ya mchujo kuwania tiketi ya kuingia hatua ya makundi katika michuano ya klabu bigwa Ulaya.

Celtic wakicheza katika uwanja wao waliibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Malmö. Mabao ya Celtic yakifungwa na leigh Griffiths aliyefunga mabao mawili na Nir Bitton , huku ya Malmo yakifungwa na Jo Berget aliyefunga mabao mawili pia.

Valencia wakiwa nyumbani Mestalla wamewachapa As Monaco kwa mabao 3-1,Daniel Parejo, Rodrigo na Sofiane wakifunga mabao ya wenyeji huku bao la Monaco likiweka kambani na Mario Pasalic

Matokeo mengine ya michezo hiyo

Basel 2 – 2 Maccabi Tel Aviv

Rapid Vienna 0 – 1 Shakhtar Donetsk

Skenderbeu Korce 1 – 2 Dinamo Zagreb