Newcastle yamsajili Florian Thauvin

Image caption Florian asajiliwa kwa mkataba wa miaka mitano

Klabu ya soka ya Newcastle United imemsajili winga Florian Thauvin, kwa mkataba wa miaka mitano kutoka Marseille ya Ufaransa.

Huku timu hiyo ikimtoa kwa mkopo kiungo wake Remy Cabella, kama sehemu ya makubaliano ya uhamisho huo.

Uhamisho huo umeigharimu Newcastle, pauni milioni 12 na kuwa mchezaji wa nne kusajiliwa katika dirisha hili la usajili.

Thauvin, aliicheza Marseille michezo 81 katika misimu miwili iliyopita na kufunga mabao 15.