Sebastian Coe aula IAAF

Image caption Sebastian Coe rais mpya wa IAAF

Bodi ya Shirikisho la riadha duniani IAAF, imemchagua Sebastian Coe kuwa rais wake mpya,katika uchaguzi huo alimuangusha Sergei Bubka kutoka Ukraine kwa kura zilizopigwa nchini China katika mji mkuu wa Beijing. Sebastian ni bingwa wa zamani wa michuano ya Olimpiki ambaye pia aliandaa michuano ya London mwaka 2012

Katika mkutano na waandishi habari, Coe hakuweka bayana juu ya suala la kitengo maalumu kitakachoanzishwa ili kupambana na tatizo la utumizi wa dawa za kuongeza nguvu michezoni.lakini akatetea uadilifu wa bodi iliyoko madarakani ,na kuahidi utendaji uliotukuka katika kuiimarisha sera ya kutokuvumilia kuhusu dawa za kulevya.