Afrobasket:Tunisia yaicharaza Uganda

Haki miliki ya picha n
Image caption Tunisia yaanza na ushindi dhidi ya Uganda

Michuano ya mpira wa kikapu Afrika yalianza jumatanao nchini Tunisia kwa wenyeji Tunisia kuanza na ushindi baada ya kuichapa Uganda kwa vikapu 77 kwa 55.

Nigeria waliwalaza Jamuhuri ya Afrika ya kati kwa vikapu 88 kwa 63.

Na katika kundi C Misri iliwalaza Gabon kwa kwa vikapu 96 kwa 49.

Huku Cameroon ikiichapa mali kwa jumla ya vikapu 70 kwa 56

Michuano hiyo inaendelea tena Alhamisi kwa michezo minne kuchezwa katika kundi B

Mabingwa watetezi Angola watacheza na Msumbiji ,Senegal wakiwakabili Morocco

huku kundi D Algeria wakiwakabili Zimbabwe na Ivory Coast wakipepetana na visiwa vya Cape Verde