Manchester City wambeba Nicolas Otamendi

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Nicolas Otamendi

Manchester City wamemsajili mlinzi wa kimataifa wa Argentina Nicolas Otamendi kutoka klabu ya Valencia kwa mkataba wa miaka mitano. Mchezaji huyo mwenye miaka 27 alitajwa katika kikosi bora cha La Liga msimu wa 2014-15 na aliisaidia nchi yake kufika fainali ya Kopa Amerika mwaka huu. ''Kuwa ndani ya klabu hii kunanifanya ni muhimu sana''alisema mlinzi huyo wa kati. Meneja wa City Manuel Pellegrini alisema ''Yupo imara, bora katika kukabiliana na wapinzani na ni bora pia kiufundi''