Ryan Jones astaafu raga.

Image caption Ryan Jones

Nahodha wa zamani wa Wales Ryan Jones amestaafu kucheza mchezo wa raga kutokana na ushauri wa madaktari.Mchezaji huyo mwenye miaka 34, aliyeshinda pia vikombe 75 katika timu yake ya Wales,amekua na nafuu kutokana na upasuaji wa bega aliofanyiwa mwishoni mwa msimu uliopita.

Lakini Jones amehsauriwa kutorudi tena katika mchezo huo kutokana na kuwepo uwezekano wa kupata majeraha makubwa zaidi jambo ambalo linaweza kuwa hatari kwake.''Maneno pamoja na umri juu ya kufanya maamuzi pamoja na kuwa na moyo mzito wa kuamini ni ukweli wa wazi katika wakati nilio nao hivi sasa''Jones alisema.

''Majuma machache yaliyopita nilikua na hisia kubwa na ngumu kwangu.Nimepata kutambua, na kuamua ukweli kuwa akili bado inahitaji lakini mwili hauwezi tena kufanya kile nilichozoea kufanya katika uwanja wa raga.

Jones anarekodi ya kuwa miongoni mwa wachezaji watatu kutoka Wales kushinda vikombe vingi katika historia ya Raga nchini humo akiwa pia na rekodi nzuri ya mwaka 2005, 2008 na 2012.