Anne Fraser Pryce ashinda mita 100

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Shelly Ann Fraser Pryce

Mwanariadha wa Jamaica Shelly-Ann Fraser-Pryce alimkabili Dafne Schippers wa Uholanzi katika utepe na kushinda mbio za mita 100 upande wa wanawake kwa mda wa sekunde 10.76.

Ilikuwa ni dhahabu ya sita kwa mwanariadha huyo kushinda baada ya kushinda mbio za mita 100 na 200 mwaka 2013.

Schippers ni bingwa wa mbio za Heptathlon baada ya kushinda medali ya shaba miaka miwili iliopita.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Beijing

Ni rekodi ya taifa kwa upande wa Schippers mwenye umri wa miaka,ambaye alianza kushiriki katika mbio fupi mnamo mwezi Juni huku Bowie mwenye umri wa miaka 24 akichukua medali yake kubwa ya kwanza.

Mwanariadha wa Nigeria aliyepigiwa upatu kufanya vizuri Blessing Ogakbare alimaliza wa mwisho.