Mourinho aanza tambo:

Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amesema matokeo ya timu yake dhidi ya West Brom yatawanyima raha wabaya wao.

Ameyasema hayo baada ya kupata ushindi wa kwanza tokea msimu mpya wa ligi ya England ianze.

Katika mchezo huo uliochezwa mwishoni mwa juma lililopita, Chelsea iliibuka kidedea kwa jumla ya bao 3-2 dhidi ya West Brom na kushuhudia nahodha wake John Terry akilimwa kadi nyekundu katika dakika ya 54 ya mchezo baada ya kumchezea vibaya mshambuliaji wa West Brom Salomon Rondon. Ushindi huu ni wa kwanza kwa Chelsea baada ya kufanya vibaya kwenye michezo miwili ya awali. Lakini pia hii ni mara ya kwanza kwa matajiri hao wa jiji la London, kufanya vibaya katika michezo miwili mfululizo ya awali katika kipindi cha miaka 17.