Beijing:Je,Wakenya watawika leo?

Image caption Rudisha

Ni siku kubwa kwa Wakenya katika mashindano ya IAAF mjini Beijing Uchina.

Nayo ni fainali ya mbio za kuruka viunzi na maji mita 3,000 mchezo ambao inautawala.

Kuna Wakenya wanne mwaka huu akiwemo mwanariadha bora katika mbio hizi mwaka huu Jarius Birech,bingwa wa dunia mara tatu Ezekiel Kembo ,bingwa wa Olimpiki mwaka 2008 Brimin Kipruto na mshindi wa medali ya Silva Consesius Kipruto.

Mtu ambaye anaweza kuingilia kati na kuinyima Kenya medali 1-2-3-4 ni bingwa wa mbio hizo nchini Marekani Evan Jager.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Usain Bolt

Vilevile Wakenya wanatarajia medali zaidi katika mbio za mita 10,000 ambapo Vivian Cheruiyot anarudi kutoka kwa likizo ya kujifungua.

Vilevile ni siku ya fainali ya mbio za mita 100 upande wa wanawake na huenda muda bora ukawekwa baada ya wanariadha kukimbia chini ya sekunde 11.

Mwanariadha wa Nigeria Blessing Okagbare ni miongoni mwa wanariadha wanaowania dhahabu.