Andy Murray , Novak wajipanga Us Open

Haki miliki ya picha PA
Image caption Andy Murray

Andy Murray amepangwa kucheza wa tatu nyuma ya Novak Djokovich na Rodger Federer kuelekea michuano ya US Open inayotarajiwa kuanza juma lijalo ambapo anajiandaa kutetea taji hilo aliloshinda mwaka 2012.

Mchezaji namba moja duniani katika mchezo wa tenisi kwa upande wa wanaume Novak Djokovich ataanza michuano hiyo ambapo atafuatiwa na mshindi mara tano wa michuano hiyo Roger Federer.

Kwa upande wa kina dada bingwa mtetezi Serena Williams ataanza akifuatiwa na Simona Halep wa Romania huku mshindi wa mwaka 2006 Maria Sharapova akiingia wa tatu.