Nigeria mabingwa kikapu

Image caption Nigeria ni mabingwa wa Kikapu Afrika

Timu ya taifa ya Nigeria ya mchezo wa kikapu imetwaa ubingwa wa mpira wa kikapu barani Afrika baada ya kuichapa Angola .

Nigeria imetwaa ubingwa wa wa Afro Basket kwa kuwagalagaza mabingwa watatezi wa michunao hiyo Angola kwa vikapu 74 kwa 65.

Mchezaji wa Nigeria Chamberlain Emeka Oguch ndiye aliyekuwa nyota wa mchezo huo baada ya kupata pointi 19 huku Abdul Wahab akipata rebaundi 12.

Wenyeji wa michuano hiyo Tunisia wamekua washindi wa tatu baada ya kuichapa Senegal kwa vikapu 82 kwa 73.