Muda wa mwisho wa usajili wanukia Uingereza

Image caption Alex Song

Leo ikiwa ni siku ya mwisho ya usajili wa wachezaji katika ligi mbali mbali za kimataifa vilabu kadhaa vinaendelea na juhudi zao wa kuwasijili wachezaji wapya ili kuimarisha vikosi vyao.

West Ham imemsajili kiungo wa kati wa Barcelona, Alex Song kwa mkopo msimu huu huku nyota wawili wa Manchester United, wakihamia Ujerumani huku kipindi cha usajili wa wachezaji kikikaribia kufungwa Uingereza.

Mshambuliaji wa Manchester United, Javier Hernandez amejiunga na Bayer Leverkusen, kwa mkataba wa miaka mitatu, mkataba unaokisiwa kugharimu dola £7.3m.

Kiungo wa kati wa Manchester United kutoka Ubelgiji, Adnan Januzaj, mwenye umri wa miaka 20, naye amejiunga na Borussia Dortmund kwa mkopo.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Adnan Januzaj

Song, mwenye umri wa miaka 27, aliyechezea Cameroon, Kombe la Dunia aliichezea West Ham msimu uliopita ambako alicheza mechi 31.

Song alijiunga na Barcelona mwaka 2012 kutoka Arsenal kwa kitita cha £15m mkataba wake ukiwa na kifungu cha kumwachilia cha £63m.

Amechezea Barcelona jumla ya mechi 39.

Wengine waliohama ni kipa wa kimataifa wa Denmark Lindegaard, 31, aliyehama Manchester United na kujiunga na West Brom kwa mkataba wa miaka miwili.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ramiro Funes Mori

Everton nao wamesajili mlinda lango Ramiro Funes Mori, kutoka klabu ya Argentina ya River Plate, kwa kitita cha £9.5m.

Mshambuliaji wa Liverpool, Fabio Borini aliyekuwa akisakwa na Inter Milan, Fiorentina na Watford naye ameihamia Sunderland.

Baada ya kupoteza wachezaji wengi, Manchester United wanakaribia kumnunua mshambuliaji wa Monaco mwenye umri wa miaka 19, Anthony Martia,l kwa kitita cha £36m, mabingwa wa ligi Uingereza Chelsea nao wakikaribia kumsajili mlinda lango Senegal Papy Djilobodji kutoka Nantes kwa mkataba unaotarajiwa kugharimu kitita cha £4m.