Timu ya raga ya AK yakumbwa na utata

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mechi ya raga ya kombe la dunia

Jaji mmoja nchini Afrika Kusini ameshutumu mwendo wa pole wa mabadiliko yanayotekelezwa katika secta ya michezo nchini humo.

Jaji Ntendeya Mavundla, alikuwa akisikiliza kesi kuhusu ikiwa wasimamizi wa mchezo wa raga nchini humo, walikuwa wamekiuka sheria wakati wa uteuzi wa timu ya taifa ya nchi hiyo.

Wasimamizi wa mchezo wa mchezo huo waliwateuwa wachezaji wengi ambao ni Wazungu.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wachezaji wa timu ya Afrika Kusini

Wachezaji tisa pekee kati ya 31 ni Waafrika.

Jaji huyo amesema mahakama haina uwezo wa kuamua ikiwa wasimamizi walivunja sheria au la, lakini amesema mabadiliko katika secta ya michezo yanatekelezwa kwa mwendo wa koba.

Mchezo wa raga ulionekana kuwa mchezo unaovutia wazungu wengi hasa baada ya taifa hilo kujinyakulia uhuru wake.

Amesema hatazuia kikosi hicho kuelekea mjini London kwa fainali za kombe la dunia ya mchezo huo.

Chama cha Agency for a New Agenda, kilikwenda mahakamani kutaka kikosi hicho kuzuiwa kwenda London kwa sababu hakikuwa na idadi tosha ya wachezaji ambao ni Waafrika