Ujerumani yashinda, Ugiriki hoi

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mashabiki wa timu ya Ujerumani

Timu ya taifa ya Ujerumani imepanda hadi kileleni mwa msimamo wa kundi D la michuano ya kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya barani Ulaya mwaka 2016 baada ya kuichabanga Poland magoli 3 - 1.

Thomas Muller ndiye aliyefungua karamu ya magoli kwa upande wa Ujerumani kwa kupachika goli la kwanza katika dakika ya 12 na baadae Mario Gotze naye akafunga magoli mawili katika dakika ya 19 na 82.

Goli pekee la Poland lilifungwa na Robert Lewandowski katika dakika ya 36.

Nayo timu ya Taifa ya Ugiriki ikajikuta ikifungwa goli 1 na Finland.

Goli pekee la Finland lilifungwa na Joel Pohjanpalo katika dakika ya 74.

Matokeo mengine ya mechi zilizochezwa hapo jana haya hapa chini

• Georgia 1 – 0 Scotland

• Ujerumani 3 - 1 Poland

• Gibraltar 0 - 4 Jamuhuri ya Ireland

• Faroe Islands 1 - 3 Ireland ya Kaskazini

• Greece 0 - 1 Finland

• Hungary 0 - 0 Romania

• Denmark 0 - 0 Albania

• Serbia 2 - 0 Armenia