Mayweather kuzichapa na Andre Berto

Image caption Mayweather

Bingwa wa ndondi katika uzani wa Welter duniani Floyd Mayweather amesisitiza kuwa pigano lake kati yake na bingwa katika uzani huo Andre Berto litamwezesha kufikia rekodi iliowekwa na Rocky Marciano ya mapigano 49 bila kushindwa.

Wengi wanaamini kwamba Mayweather mwenye umri wa miaka 38 hawezi kushindwa kuvunja rekodi hiyo ya Marciano lakini mwenyewe anasema kuwa afya yake ni muhimu zaidi.

''Ukisalia ulingoni kwa mda mrefu chochote chaweza kutokea'', alisema Mayweather.''Sijali kuhusu kushindwa ,lakini bado najali kuwa na afya njema.

''Unaweza kutengeza fedha chungu nzima lakini muhimu ni kuweza kutembea na kuzungumza.Pigano la 49 ndio pigano langu la mwisho'',alisema.