Serena William apata pigo

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Serena katika mkutano na vyombo vya habari baada ya mechi hiyo.

Bingwa wa mchezo wa tenisi upande wa wanawake Serena Williams amepata pigo kubwa katika mashindano ya US Open baada ya kushindwa kwa seti 2-6 6-4 6-4 na Muitaliano Roberta Vinci katika nusu fainali.

''Ni pigo kubwa'', alisema aliyekuwa bingwa mara mbili katika mchezo huo Tracy Austin.

''Hili ni pigo kubwa katika historia ya mchezo huu kutokana na kile kilichofanyika''.

Haki miliki ya picha All Sport
Image caption Serena akisalimiana na Vinci baada ya mechi hiyo

William alianza mechi hiyo akiwa hajashindwa katika mechi 33 katika Grand Slum tangu machindano ya Wimbledon ya mwaka 2014.

Alikuwa amejitahidi kufikia rekodi iliowekwa na Steffi Graf ya mwaka 1988 ambapo mwana dada huyo alizoa mataji yote mwaka huo na alikuwa akikabiliana na mchezaji ambaye alimshinda mara nne bila kushindwa seti moja.