Adebayor aondoka Tottenham

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Adebayor

Mshambuliaji wa kilabu ya Tottenham Emmanuel Adebayor ameondoka katika kilabu hiyo baada ya makubaliano ya pande zote mbili.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 kutoka Togo alikuwa hajaichezea Spurs msimu huu na alikuwa amewachwa katika vikosi vya kucheza ligi ya Uingereza pamoja na ile ya Yuropa.

''Tunamuombea mema katika maisha yake ya baadaye',ilisema taarifa ya Tottenham.

Adebayor aliyewasili katika kilabu ya Manchester City kwa kitita cha pauni milioni 5 mwaka 2012,alikuwa amesalia na mwaka moja katika kandarasi yake na alikuwa akitaka kulipwa pauni milioni 5 ili kusitisha kandarasi hiyo mapema.

Hatahivyo kilabu ya Tottenham haijatangaza makubaliano ya usitishwaji wa kandarasi hiyo.

Akizungumza mapema juma hili ,kocha mkuu wa Tottenham Mauricio Pochettino alisema kuwa Adebayor hakuwa katika 'fikra zake' ama hata mpango wa mbeleni wa timu ya Tottenham.