Spurs, Leicester zapeta Epl

Image caption Ryan Mason aliipa ushindi wa kwanza Spurs, Epl

Wakicheza ugenini katika dimba la light timu ya soka ya Tottenham imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Sunderland.

Bao la Dakika ya 82 la kiungo Ryan Mason limewapa Spurs ushindi wa kwanza kwenye Ligi Kuu England baada ya Mechi 5 wakiwa na pointi 6 katika nafasi ya 12.

Nao Leicester City, Timu iliyopanda Daraja Msimu huu, imeendeleza wimbi lao la ushindi baada ya kuichapa Aston Villa kwa mabao 3-2.

Villa walianza kupata bao kupitia Chipukizi Jack Grealish na Carles Gil kuongeza bao la Pili.

Lakini Ritchie de Laet na mshambuliaji Jamie Vardy wakachomoa mabao hayo kabla ya Nathan Dyer kufunga bao la tatu na la ushindi .

Ligi hiyo itaendelea tena leo kwa mchezo mmoja kupigwa kwa West Ham kuwakabili Newcastle United katika dimba la Upton Park.