Djockovic bingwa US Open

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Bingwa namba moja mchezo wa Tenisi duniani, Novak Djockovic

Nyota namba moja duniani kwa mchezo tenesi Novack Djockovic ametwaa taji la Us Open baada ya kumshinda mpinzani wake Rodger Federer anayeshika nafasi ya pili kwa ubora duniani.

Novak ameshinda Federer kwa jumla kwa seti 6-4 5-7 6-4 6-4 kwa ushindi huu mchezaji huyo ametwaa Grand slam ya tatu kwa mwaka huu.

Na ikiwa ni Grand slam yake ya kumi katika maisha yake ya uchezaji Tenesi .

Kwa upande wa wanawake muitaliano Flavia Pennetta alitwaataji la US Open kwa wanawake baada ya kumchapa muitaliano mwenzake Roberta Vinci

Flavia alishinda kwa seti 7-6 7-4 6-2 baada ya ushindi huo nyota huyu mwenye miaka 33 akatangaza kustaafu mchezo huo.