Epl:West Ham yaichapa Newcastle

Image caption West Ham na Newcastle wakichuana,ligi kuu England

Timu ya Soka West Ham imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Newcastle katika mchezo wa ligi kuu ya England.

Kiungo mfaransa Dimitri Payet ndio aliyepeleka majonzi kwa Newcastle baada ya kufunga mabao mawili la kwanza dakika ya 9 kisha akaongeza bao la pili dakika 48.

Newcastle United walitawala mchezo kwa asilimia kubwa wakimiliki mchezo huo kwa asilimia 61 huku West Ham wakimiliki kwa asilimia 39.

Kwa ushindi huo unawafanya wagonga nyundo hao wa London kushika nafasi ya tano katika msimamo wa ligi wakiwa na alama 9 baada ya kucheza michezo mitano.