UEFA: Man United, Man City zachapwa

Image caption Man City ikikipiga na Juventus

Timu za Uingereza za Man United na Man City zimeanza vibaya michuano ya kombe la kilabu bingwa barani Ulaya baada ya kuchapwa.

Man United wakiwa ugenini nchini Uholanzi wamelala kwa kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya PSV. Memphis Depay alianza kuifungia timu yake bao la kwanza kabla ya Héctor Moreno wa PSV kusawazisha kisha Luciano Narsingh akafunga bao la ushindi.

Man City nao wakiwa katika dimba lao la Etihad walikubali kipigo cha mabao 2-1 toka kwa vibibi vizee vya Turin Juventus mabao ya Juve yakifungwa na Álvaro Morata na Mario Mandzukic huku bao la kujifunga la beki Giorgio Chiellini, likiwapa Man City bao moja.

Real Madrid wakiwa nyumbani Santiago Bernabeu wameshinda kwa kishindo kwa ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Shakhtar Donetsk, Cristiano Ronaldo akifunga hat trick na Karim Benzema akifunga bao moja.

Matokeo mengine ya michuano hii ni:

PSG 2 – 0 Malmö FF

VfL Wolfsburg 1 – 0 CSKA

Benfica 2 – 0 FC Astana

Galatasaray 0 – 2 Atletico Madrid

Sevilla 3 – 0 Borussia Mönchengladbach