Wenger: Walcott ndiye tegemeo letu

Image caption Wenger

Arsenal inaanza kampeni yake katika michuano ya vilabu bingwa Ulaya siku ya jumatano ikiwa itakabiliana na Dinamo Zagreb katika uwanja wa Stadio Maksimir.

Mkufunzi Arsene Wenger amekuwa akikosolewa kwa kushindwa kununua mshambuliaji mpya, lakini anasema kuwa anakiamini kikosi chake na kwamba Theo Walcott ndio jibu la safu yake ya mashambulizi.

Pia amesema kuwa ni muhimu kwa kikosi chake kutoshindwa katika mechi ya kwanza ya michuano hiyo nchini Croatia.