Arsenal yachapwa,Chelsea yashinda

Timu ya soka ya Arsenal ikicheza ugenini imekubali kuchapwa 2-1 na timu ya Dinamo Zagreb katika mchezo wa klabu bingwa barani ulaya, Oxlade-Chamberlain alianza kujifunga kisha Junior Fernandes huku bao la Arsenal likifungwa na Theo Walcot.

Chelsea wakicheza nyumbani walipata ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Maccabi Tel Aviv mabao yakifungwa na Williani,Oscar, Diego Costa na kiungo Cerc Fàbregas akifunga bao la mwisho.

Huko italy Roma wakiwa wenyeji wa Barcelona wamekwenda sare ya kufunga bao 1-1.

Matokeo ya michezo mingine iliyopigwa ni

Bayer Leverkusen 4 –1 bBATE Bor

Olympiakos 0 – 3 Bayern Mun

Dynamo Kiev2 - 2FC Porto

KAA Gent 1 – 1 Lyon

Valencia 2 – 3 Zenit St P