Wagombea wa michezo ya Olimpiki 2024 watangazwa

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Olimpiki 2024

Wanaogombea kuandaa mashindano ya michezo ya Olimpiki mnamo mwaka 2024 wametangazwa.

Miji hiyo ni pamoja na Paris- Ufaransa, Roma- Italia, Los Angeles nchini Marekani, Budapest pamoja na Hamburg.

Maamuzi ya mwisho yatatangazwa nchini Peru katika mkutano wa kamati kuu ya Olimpiki katika kipindi cha miaka miwili ijayo.

Mwaandishi wa habari za michezo wa BBC , anasema kuwa miji miwili ambayo inapigiwa upatu wa kuteuliwa ni Paris na Los Angeles.