Spurs, Borussia zaanza kwa ushindi

Image caption Spurs yaanza kwa ushindi,ligi ya Europa

Michuano ya Europa ligi imeanza rasmi kwa msimu wa 2015-2016 huku ikishudia timu za Tottenham,Schalke na Borrusia Dortimund wakianza kwa ushindi.

Tottenham wakiwa nyumbani kwenye dimba la White hart lane waliibuka na ushindi wa mabao 3 – 1 dhidi ya FK Qarabag.

Apoel Nicosia wakiwa wenyeji wa Schalke walikubali kuchapwa kwa 3-0, wajerumani wa Borrusia Dortmund wakashinda kwa mabao 2 – 1 dhidi ya FK Krasnodar.

Matokeo mengine ya michuano hii

Ajax 2 – 2 Celtic

Bordeaux 1 – 1 Liverpool

Fenerbahçe 1 – 3 Molde

Anderlecht 1 – 1 Monaco

Asteras Tripolis 1 – 1 Sparta Prague

Ath Bilbao 3 – 1 FC Augsburg

Partizan Belgrade 3 – 2 AZ Alkmaar

FC Sion 2 – 1 Rubin Kazan

FK Qabala 0 – 0 PAOK Salonika