Luke Shaw kufanyiwa upasuaji

Mlinzi wa kushoto wa Man United Luke Shaw atafanyiwa upasuaji wa pili leo katika mguu wake uliovunjika.

Shaw yuko katika hospital ya St Anna Ziekenhuis alikopelekwa mara baada ya kuvunjika mguu katika mchezo wa ligi ya mabigwa dhidi ya PSV.

Nyota huyu aliumizwa na beki Hector Moreno dakika ya 15 ya mchezo, familia ya mchezaji huyo imekwenda Uholanzi kumuangalia chipukizi huyo.

Beki huyu kisiki wa upande wa kushoto ataukosa msimu mzima wa ligi na anatarajiwa kurejea uwanja tena mwezi Machi mwakani.