FIFA:Viongozi 2 Afrika Kusini mashakani

Haki miliki ya picha
Image caption Barua ya Afrika kusini kwa FIFA

Kiongozi wa maandalizi ya kombe la dunia nchini Afrika Kusini mwaka 2010 ni miongoni mwa maafisa wawili wakuu waliotajwa katika malalamishi ya uhalifu yanayodai kufanyika kwa ufisadi katika kura ya FIFA ilioamua atakayeandaa dimba hilo.

Chama rasmi cha upinzani nchini Afrika Kusini ,Demokratic Alliance kimesema kuwa kimewataka maafisa wa polisi siku ya jumatatu kuchunguza kuhusika kwa kiongozi wa maandalizi ya kombe la dunia nchini Afrika kusini Danny Jordan na rais wa shirikisho la soka nchini humo Molefi Oliphant kwa madai ya kutoa hongo ili kupewa maandalizi ya kombe hilo.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Aliyekuwa rais wa Afrika kusini Thabo Mbeki akipokea kombe la dunia kutoka kwa Sepp Blatter

Chama hicho kinasema wawili hao wanapaswa kuchunguzwa kuhusu malipo ya dola milioni 10 kwa Jack Warner ,aliyekuwa afisa mkuu ambaye ameshtakiwa na mahakama moja ya Marekani kwa hongo na kujihusisha na biashara zisizo halali.

Mamlaka ya Marekani inayochunguza ufisadi katika shirikisho la soka duniani FIFA inasema kuwa aliyekuwa afisa mkuu wa FIFA Chuck Blazer alikiri kwamba fedha hizo zilikuwa hongo ya maandalizi hayo kufanywa Afrika Kusini.