Diego Costa ashitakiwa

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Diego Costa

Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa ameshtakiwa kwa madai ya kutaka kuzua ghasia ambayo haya kuonekana na maafisa wa mechi hiyo lakini ambayo yalinaswa katika mkanda wa video.

Mshambuliaji huyo alihusishwa katika kisa na beki wa Arsenal Laurent Koscielny katika dakika ya 43 ya mechi.

Naye Beki wa Arsenal Gabriel Paulista ameshtakiwa kwa utovu wa nidhamu kwa tabia yake wakati alipopewa kadi nyekundu huku Santi Carzola akionywa kuhusu tabia yake mbaya.