Mourinho:'Kulipiza kisasi inakubalika EPL'

Haki miliki ya picha PA
Image caption Mourinho

Shirikisho la soka nchini Uingereza FA limeweka mfano mbaya kwa kubadilisha uamuzi wa kadi nyekundi aliyopewa beki wa Arsenal Gabriel Paulista kulingana na kocha wa Chelsea Jose Mourinho.

Beki Gabriel Paulista alipigwa kadi nyekundu kwa kumpiga teke Diego Costa wakati Chelsea ilipoibuka mshindi kwa mabao 2-0 dhidi ya Arsenal katika mechi ya ligi kuu ya Uingereza siku ya jumamosi.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Gabriel na Costa

Mourinho :''Sasa twajua kwamba kulipiza kisasi kunakubalika.Hakuna neno, unaweza kufanya''.

Costa alipigwa marufuku kwa kuzua ghasia katika kisa na beki mwenmgine wa Arsenal Laurent Koscielny kilichosababisha Gabriel kupigwa kadi nyekundu.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Diego Costa

Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa hatua ya kumpiga marufuku Costa ilisahihisha asilimia 5 pekee ya ya makosa yaliosababisha timu yake kushindwa katika uwanja wa Stamford Bridge.

Mourinho alisema kuwa hakuzungumzia swala la kupigwa marufuku ya mechi tatu kwa Costa kwa hofu ya kupewa marufuku.