Tennis:Uingereza kuivaa Japan 2016

Haki miliki ya picha PA
Image caption Mcheza Tennis maarufu Andy Murray

Uingereza inatarajiwa kukipiga na Japan katika raundi ya kwanza kwenye michuano ya Davis Cup mwaka 2016. Hata hivyo Uingereza itakuwa mwenyeji wa Japan machi 4 na 6 mwakani, kutokana na droo iliyofanyika nchini Chile.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Novak Djokovic

Ikiwa Uingereza watafanikiwa kupita katika raundi hiyo watakutana na Serbia ama Kazhakstan katika raundi ya pili.

Katika ratiba hiyo Uingereza walipewa nafasi kubwa kupangwa ndani ya droo hiyo baada ya kuwa timu ya juu kufika fainali za mwaka huu.

Uswisi nao pia wamepewa nafasi sawa na ile ya Uingereza,ambapo nyota wakubwa katika mchezo huo watakutana tena akiwemo Andy Murray, Novak Djokovic na Roger Federer.