Raga: Australia yaanza vyema

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Michuano ya Ragga 2015

Katika michuano ya kombe la Dunia kwa upande wa raga, timu ya taifa ya Australia imeshinda mchezo wake wa kwanza kwa kuifunga Fiji 28-13.

Licha ya kutoa upinzani mkali, wachezaji wa Fiji hawakuweza kuipita ngome ya wachezaji wa Australia kirahisi. Timu ya Ufaransa imeifunga Romania 38-11.

Mapema matumaini ya Japan kuendelea na ushindi baada ya kuwashangaza wengi kwa kuwatoa Afrika Kusini yalikwama baada ya kuchabangwa na Scotland 45-10.