FIFA yaanika siri za Jerome Valcke

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Jerome Valcke siri zake zawekwa wazi

Waendesha mashitaka wa Uswisi wamethibitisha kwamba shirikisho la soka duniani, FIFA ,limekubali kuweka wazi akaunti ya barua pepe mali ya Jerome Valcke ambaye ni katibu Mkuu wa FIFA .

Alifukuzwa wiki iliyopita kufuatia madai kwamba alihusika katika mpango wa kuuza tiketi za Kombe la Dunia kwa thamani ya juu.

Wanasheria wa Valcke wamekanusha madai ya mteja wao kuhusika katika tukio hilo.

Maafisa wa Uswisi wameanzisha uchunguzi wa rushwa sambamba na Idara moja ya Haki ya Marekani, ambayo ina washitaki maafisa kumi wa soka kwa tuhuma za rushwa. Jerome Valkce ni kiongozi wa juu kabisa wa FIFA anayetuhumiwa kwa rushwa.