Mancity yalala,Arsenal na Man U zashinda

Image caption sanchez
Image caption Tottenham

Manchester City imepoteza mechi ya pili mfulululizo huku Harry Kane akifunga bao lake la kwanza msimu huu na kuiwezesha Tottenham kutoka nyuma na kuichapa Manchester City mabao 4-1.Kevin De Bryune alianza kuifungia Manchester City huku Toby Alderweired ,Erik Lamela ,Christian Eriksen na Lamela akifunga udhia.Wakati huohuo Arsenal imeicharaza Leicester mabao 5 kwa mbili katika mechi iliochezwa kwa kasi ya hali ya juu.Alexi Sanchez aliifungia Arsenal mabao matatu huku Walcot na Giroud wakifunga bao moja kila mmoja.Manchester United nayo imepata ushindi wa mabao matatu kwa bila dhidi ya Sunderland huku Rooney ,Depay na Mata wakifunga.