Gabriel apewa marufuku ya mechi moja

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Gabriel Paulista

Beki wa Arsenal Gabriel Paulista amepewa marufuku ya mechi moja na kupigwa faini ya pauni 10,000 baada ya kukiri shtaka la shirikisho la soka nchini Uingereza FA la utovu wa nidhamu.

Gabriel mwenye umri wa miaka 24 alipewa kadi nyekundu na refa Mike Dean kwa kuzua ghasia alipozozana na mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa wakati wa ushindi wa Chelsea wa 2-0 dhidi ya Arsenal katika uwanja wa Stamford Bridge.

Arsenal ilikata rufaa na kufanikiwa dhidi ya marufuku ya mechi tatu kwa kadi hiyo nyekundu.

Shtaka hilo linatokana na mchezaji huyo kutoondoka uwanjani mara moja baada ya kupewa kadi hiyo.