FIFA:Blatter na Platini wachunguzwa

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais wa FIFA Sepp Blatter na rais wa UEFA Michel Platini wachunguzwa

Rais wa FIFA Sepp Blatter na rais wa UEFA Michel Platini wanachunguzwa na kamati ya nidhamu ya FIFA.

Haya yamewadia baada ya thibitisho kutoka kwa mwanasheria mkuu wa Switzerland kuwa ameanzisha uchunguzi dhidi ya wawili hao.

Blatter anakabiliwa na mashtaka mawili makuu,kutoa kandarasi ambazo zingeigharimu FIFA na kutoa malipo ya zaidi ya Franka milioni mbili za uswisi kwa rais wa UEFA Platini.

Mawakili wa Blatter wamesema kuwa wao hawana wanaloficha na kuwa watashirikiana kikamilifu na afisi ya mkuu wa sheria.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Switzerland imeanzisha uchunguzi dhidi ya wawili hao

Rais huyo wa FIFA amekanusha madai dhidi yake.

Platini -ambaye alikuwa ni mshauri wa kiufundi wa Blatter kati ya mwaka wa 1999 na 2002 anatarajiwa kutoa ushahidi dhidi yake.

Raia huyo wa Ufaransa ambaye anawania kumrithi Blatter amekanusha madai yanayomkabili ijapokuwa ameshindwa kueleza kikamilifu kwanini malipo hayo yamecheleweshwa kwa miaka tisa !