Blatter asema hatojiuzulu FIFA

Haki miliki ya picha PA
Image caption Blatter

Rais wa shrikisho la soka duniani Sepp Blatter amesema kuwa hatojiuzulu wadhfa wake licha ya mashtaka ya uhalifu yanayofungiliwa dhidi yake na wachunguzi wa Uswizi.

Raia huyo wa Usiwizi aliye na umri wa miaka 79,anatuhumiwa kutia saini kandarasi ambayo haikuifaa FIFA mbali na kufanya malipo yasiokubalika kwa rais wa shirikisho la UEFA Michel Platini .

Blatter ambaye atajiuzulu kama rais wa FIFA mwezi Februari anasema kuwa hajafanya kosa lolote kinyume na sheria.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Blatter na Platini

Platini mwenye umri wa miaka 60,amendika barua kwa wanachama wa UEFA akikana kufanya kosa lolote.

Katika taarifa iliotolewa na mawakili wake,Blatter amesema kuwa pauni milioni 1.5 zilizotolewa kama malipo kwa Platini ,ambaye ndio kiongozi wa shrikisho la soka barani Ulaya UEFA mwaka 2011 ni halali na hakuna zaidi.

Wawili hao pia wanakabiliwa na uchunguzi na kamati ya maadili ya FIFA kuhusu malipo hayo ambayo Platini anasema yalikuwa ya kazi wakati alipokuwa mshauri wa kiufundi wa Blatter kati ya mwaka 1999 na 2002.