Majeraha yamuandama Sharapova

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Maria Sharapova

Nyota wa tenesi Maria Sharapova ameendelea kuandamwa na majeraha baada ya kuumia kwenye michuano ya wazi ya Wuhan huko China.

Sharapova alikua akicheza mchezo wake wa kwanza baada ya kupona majeraha ya mguu yaliyomuweka nje ya uwanja kwa muda, huku ukiwa ni mchezo wa kwanza toka alipopoteza mchezo dhidi ya Serena Williams katika nusu fainali ya michuano ya Wimbledon mwezi Julai.

Katika mchezo huo Sharapova alishinda kwa seti 7-6 (7-1) 6-7 (4-7) 2-1 dhidi ya Barbora Strycova.

"Nimepata maumivu tena katika mguu wangu wa kushoto ni hali mbaya inaendealea"alinukuliwa Sharapova baada ya kumaliza mchezo huo.