Fifa: Argentina bora duniani

Image caption Kikosi cha timu ya taifa la Argentina

Shirikisho la soka duniani Fifa limetangaza viwango vya ubora vya mchezo wa soka kwa mwezi Septemba ambapo taifa la Argentina limeendelea kuongoza katika chati hiyo.

Mabingwa wa dunia Ujerumani wako nafasi ya pili, Ubelgiji wanashika nafasi ya tatu katika viwango vya ubora.

Algeria ndio taifa la Afrika linaloongoza likiwa nafasi ya 19 huku Ivory Coast wakiwa nafasi ya 21 .

Kwa upande wa Afrika mashariki Uganda wako juu wakiwa nafasi ya 75,Rwanda iko katika nafasi ya 93 huku Burundi wakijichimbia katika nafasi ya 113, kenya wao wako nafasi ya 131 na Tanzania ikiwa nafasi ya 136.

Orodha ya kumi bora

1 Argentina

2 Germany

3 Belgium

4 Portugal

5 Colombia

6 Spain

7 Brazil

8 Wales

9 Chile

10 England