Serena Williams kupumzika kwa mwaka

Haki miliki ya picha All Sports
Image caption Mcheza tenisi namba moja kwa ubora duniani,Serena Williams

Mcheza tenesi namba moja kwa ubora duniani kwa upande wa wanawake Serena Williams atapumzika kucheza mchezo huo kwa mwaka mzima kutoka na kuwa na majeraha.

Mshindi huyo wa Grand Slam 21 alitolewa kwenye michuano ya wazi ya Wuhan ,Williams mwenye miaka 34 amesema" nimecheza nikiwa na maumivu kwa muda wa mwaka mzima,"

Nyota huyo wa tenesi tayari ametoa taarifa ya kupumzika kwa chama cha mchezo wa tenesi kwa wanawake(WTA)

Serena msimu huu wa 2015 ameshinda mataji ya wazi Australian French Open na lakini haja cheza toka alipofungwa na Muitaliano Roberta Vinci.